Pata taarifa kuu
MISRI

Kesi ya Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak kusikilizwa tena mwezi June

Rufaa ya kesi dhidi ya mauaji ya waandamanaji inayomkabili Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak imesogezwa mbele na itasikilizwa tena tarehe 8 ya mwezi june ili kuwapa majaji muda zaidi wa kupitia ushahidi mpya uliowasilishwa kwao.

AFP PHOTO/EGYPTIAN TV
Matangazo ya kibiashara

Mubarak sambamba na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wakati wa utawala wake Habib al-Adly na maofisa sita wa usalama walifikishwa mahakamani jana jumamosi na kusomewa mashtaka ya rushwa na mauaji ya waandamanaji yaliyotekelzwa wakati wa harakati za kumuondoa madarakani Bwana Mubarak.

Mahakama ya Misri iliamuru kusikilizwa upya kwa kesi hiyo baada ya upande wa Mubarak kupinga hukumu ya awali ya kifungo cha maisha iliyotolewa mwezi June mwaka jana.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa upya tarehe 13 ya mwezi April mwaka huu lakini ilishindikana baada ya Jaji Mostafa Hassan Abdallah kujiondoa mwenyewe katika mwendelezo wa kesi hiyo.

Watoto wawili wa Mubarak Gamal na Alaa nao wanakabiliwa na mashtaka ya rushwa sambamba na baba yao.

Watu zaidi ya mia nane waliuawa katika machafuko hayo yaliyoshika kasi nchini humo mwaka 2011 na kufanikisha kuuangusha utawala wa Mubarak.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.