Pata taarifa kuu
MISRI-MAANDAMANO

Harakati za kumng'oa madarakani Rais Mohammed Morsi zazidi kushika kasi nchini Misri

Maelfu ya waandamanaji wa upinzani wameendelea kukusanyika katika viwanja vya Tahrir mjini Cairo kwa lengo la kushiriki maandamano makubwa yanayofanyika jumapili hii kushinikiza kuondoka madarakani kwa Rais wa Misri Mohammed Morsi.

REUTERS/Asmaa Waguih
Matangazo ya kibiashara

Maandamanao hayo yanafanyika leo siku ambayo ni ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu Morsi achaguliwe kuwa Rais wa Misri baada ya kufanikiwa kwa mapinduzi ya kisiasa ya mwaka 2011 yaliyouangusha utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak.

Wafuasi wa Rais Morsi nao wamekusanyika kwa lengo la kuadhimisha mwaka mmoja kwa kiongozi wao kuwa madarakani huku wakiahidi kuendelea kuunga mkono utawala wake.

Hofu imezidi kutanda katika mitaa mbalimbali ya nchi hiyo hasa baada ya kuuawa kwa watu watatu akiwamo raia mmoja wa Marekani aliyeuawa wakati akiwapiga picha waandamanaji siku ya ijumaa.

Marekani, Ufaransa na mataifa mengine yameendelea kutoa wito kwa raia wake waliopo Misri kujiepusha na mikusanyiko isiyo na lazima kwao na kuwataka wengine kutoingia nchini humo kwa sasa.

Wapinzani wa Rais Morsi wanasema watu zaidi ya milioni ishirini na mbili wametia saini azimio la kuitishwa kwa uchaguzi mwingine na takwimu zaidi zinatarajiwa kutolewa hii leo katika viwanja vya Tahrir.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.