Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Rais Mugabe atishia kulipiza kisasi dhidi ya kampuni za Marekani na Uingereza

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameyaonya mataifa ya Magharibi kuwa atalipiza kisasi dhidi yao ikiwa yataendelea kuiwekea nchi yake vikwazo vya kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Mugabe ambaye aliapishwa wiki iliyopita kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa saba amesema kuwa huenda akazichukulia hatua kampuni zinamilikiwa na serikali ya Marekani na Uingereza nchini humo ikiwa vikwazo dhidi ya nchi yake vitaendelea kuwepo.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 89 ameongeza kuwa wananchi wa Zimbabwe wanashangazwa namna wanavyoteswa na mataifa hayo ya Magharibi wakati wao wakiishi vizuri na raia wa kigeni.

Kiongozi huyo wa Zimbabwe amesema ni lazima kuwe na usawa ili kuwaruhusu wawekezaji wa kigeni kuja nchini humo, na kuongeza kuwa wakati wa nchi yake kuwekewa vikwazo umepita.

Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya waliiwekea vikwazo vya kiuchumi  serikali ya Zimbabwe pamoja na washirika wa karibu wa rais Mugabe kuanzia mwaka 2002 baada ya Uchaguzi Mkuu ambao mataifa hayo yalisema haukuwa huru na haki.

Juhudi za Mugabe pia zimeungwa mkono na muungano wa mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC ambayo pia yanataka vikwazo kuondolewa dhidi ya mwanachama wake.

Mapema mwaka huu, Umoja wa Ulaya ulitangaza kumwondelea vikwazo vya kusafiri rais Mugabe lakini inaendelea kushikilia vile  vya kiuchumi.

Marekani inasema ni sharti Mugabe aanze mchakato wa kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo ili kuimarisha demokrasia ya kweli .

Uchaguzi Mkuu uliofanywa kwezi uliopita ullikosolewa pakubwa na Mataifa ya Magharibi huku upinzani ukiongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Morgan Tsangirai ukidai kuwa kura ziliibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.