Pata taarifa kuu
TANZANIA-KATIBA

Hatimaye bunge maalum la katiba nchini Tanzania lampata mwenyekiti wa kudumu

Bunge maalum la katiba nchini Tanzania, limemchaguwa jana Samuel Sitta kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge hilo, hatuwa ambayo imekuja baada ya kupasishwa kwa kanuni ambazo zitawaongoza wajumbe hao kujadili rasimu ya katiba. Waziri huyo wa Afrika Mashariki, amechaguliwa kwa kishindo kuliongoza Bunge Maalumu la Katiba, huku akisema kuchaguliwa kwake ni sawa na kumrudisha chura kwenye dimbwi la maji.

Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge maalum la katiba.
Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge maalum la katiba. RFI
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia hatuwa hiyo, bunge la katiba linatarajiwa kuanza rasmi mijadala juu ya kujadili katiba baada ya kupatikana kwa viongozi.

Baada ya hatuwa hiyo ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge la katiba, Samuel Sitta aliwashukuru wabunge kwa kumchaguwa.

Samuel Sitta ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Urambo mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alipata kura 487 na kumshinda mpinzani wake, Hashimu Rungwe wa Chama cha Ukombozi wa Umma aliyepata kura 69.

Wajumbe wengine, Dk. Terezya Huvisa pia wa CCM na John Chipaka wa Tadea, walijitoa katika kinyang’anyiro hicho ambacho tangu awali Sitta alionyesha kujiandaa kwa kutengeneza vipeperushi alivyovisambaza kwa wajumbe kama sehemu ya kujinadi.

Sitta alionekana kujiamini kabla na baada ya uchaguzi.

Sitta amesema kwamba amejaa na “falsafa “ ya chura, akimaanisha kuwa wajumbe wamemchagua mtu mwenye uwezo, uzoefu na weledi wa kuongoza shughuli za bunge.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wanaona kuwa mwenyekiti wa kudumu wa bunge la katiba anakabiliwa na changamoto mbalimbali na kuhakikisha rasimu ya katiba inapatikana kwa wakati.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.