Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-Siasa

Afrika Kusini: baraza jipya la mawaziri latangazwa

Rais Jacob Zuma ametangaza baraza jipya la mawaziri na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, wizara ya fedha itaongozwa sasa na waziri kutoka jamii ya watu weusi.

South Africa's President Jacob Zuma celebrates his re-election as ANC Party President in Bloemfontein, 18 December, 2012
South Africa's President Jacob Zuma celebrates his re-election as ANC Party President in Bloemfontein, 18 December, 2012 Reuters/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Matamela Cyril Ramaphosa ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa chama cha ANC ndiye aliyeteuliwa makamu wa rais wa Afrika Kusini kuisaidia serikali ya Zuma kutekeleza ajenda yake ya mageuzi ya kijamii na ya kiuchumi aliyoahidi wakati wa kampeni yake ya uchaguzi.

Aidha, Nhlanhla Nene mwenye umri wa miaka 55 ambaye alikuwa mkurugenzi wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2010 na naibu waziri wa fedha tangu 2009 ndiye sasa ataongoza wizari ya fedha na ambaye atakuwa na wajibu wa kutekeleza mabadiliko ya kiuchumi.

Katika hotuba yake alipoapishwa mwishoni mwa juma lililopita, Jacob Zuma alitangaza kuundwa kwa wizara hio kwa ajili ya maendeleo ya biashara ndogo ndogo, muhimu kwa sekta ya uchumi.

Mabadiliko mengine ni pamoja na uundwaji wa wizara ya maendeleo vijijini na sera mpya ya ardhi kupambana dhidi ya ukosefu wa ajira na kukosekana kwa usawa kunaoathiri watu katika maeneo ya vijijini Afrika Kusini.

Baraza hilo la mawaziri lina mawaziri 35 na manaibu mawaziri 37 .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.