Pata taarifa kuu
DRCongo-Katiba

Mpango wa marekebisho ya katiba wazua hofu jijini Kinshasa

Viongozi wawili wa upinzani nchini DRCongo, wameituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kuandaa muswada wa marekebisho ya katiba ikiwa ni siku moja baada ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutangaza kwamba imeridhia pendekezo la marekebisho ya katiba ili kuwezesha maandalizi ya uchaguzi ujao kuanzia ngazi ya serikali za mtaa hadi uchaguzi wa rais, baada ya kikao cha baraza la mawaziri kisischokuwa cha kawaida kilichofanyika jijini Kinshasa. 

Uchaguzi mkuu wa rais nchini DRCongo unatarajiwa kufanyika mwaka 2016
Uchaguzi mkuu wa rais nchini DRCongo unatarajiwa kufanyika mwaka 2016 AFP PHOTO/ ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Albert Moleka mkurungezi wa chama cha UDPS cha Ethienne Tshisekedi amesema mbinu zote ni kutaka kuwapa njia viongozi wa sasa nchini humo kuwani auchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo halikubaliki.

Upande wake Vital Kamerhe wa chama cha UNC, amesema hatuwa hii inasikitisha sana na ni uhaini na ni jambo lisilokubalika.

Katika taarifa iliyosomwa na waziri wa mawasiliano na msemaji wa serikali hiyo Lambert Mende Omalanga, azimio hilo limepitishwa na baraza la mawaziri ili kurekebisha kasoro za msingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi wa wabunge na wa rais mwaka 2011, bila hata hivo kuweka bayana vipengele ambavyo vitafanyiwa marekebisho.

Hata hivyo kumekuwa na hofu upande wa upinzani wa kufanyika kwa mageuzi ambayo yafaufanya uchaguzi wa rais na wa bunge isiwi wa moja kwa moja kama ilivyo kwa sasa, jambo ambalo linaweza kuvuruga utaratibu mzima wa uchaguzi.

Wiki kadhaa zilizopita, mijadala iliyogubikwa na hisia kali imeonyesha kuwa vyama vya upinzani nchini DRCongo vimepinga marekebisho yoyote ya Katiba na kubaini kuwa marekebisho ya aina yoyote yatalenga kumruhusu rais kabila anayemaliza muula wake wa pili kuwania urais kinyume na katiba iliopo.

Mwaka 2011, Katiba ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilirekebishwa ili pasiwepo na duru ya pili ya uchaguzi wa rais, jambo ambalo limelalamikiwa na wadau wa kisiasa na hata wa kidini na kuituhumu Tume ya Uchaguzi kuegemea upande wa rais Kabila.

Hivi majuzi, ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya kwa ukanda wa Maziwa Makuu umesisitiza kutangazwa kwa kalenda ya chaguzi zote, huku mjumbe maalum wa Marekani katika ukanda wa maziwa makuu Russ Feingold akielezea msimamo wa serikali ya Washington kumtaka rais kabila asigombee tena urais, jambo ambalo limekosolewa na serikali ya Kinshasa.

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.