Pata taarifa kuu
BURUNDI-AMNESTY INERNATIONAL-SUDAN-Haki za binadamu

Amnesty International yaituhumu polisi ya Sudan

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linashtumu jeshi la polisi nchini Sudan, kuwaua, kuwajeruhi na kuwatesa waandamanaji jijini Khartoum.

Maandamano ya raia katika mji wa Khartoum, nchini Sudani.
Maandamano ya raia katika mji wa Khartoum, nchini Sudani. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International imesema waandamanaji hao waliokuwa wanaadamana kwa amani kupinga kupanda kwa maisha nchini humo walizuiliwa, na kuteswa na maafisa wa usalama, tuhma ambazo Khatroum inakanusha.

Manar Idriss mmoja wa watafiti wa shirika hilo nchini Sudan amesema uchunguzi wao umebaini kuwa idaiid kubwa ya waandamanaji waliopitia mateso hayo ni vijana chini ya miaka 18 na wengine waliuawa kwa kupigwa risasi kichwani.

Ripoti ya Manesty International inaeleza kuwa vitendo hivi vimekuwa vikitekelezwa kwa zaidi ya miaka miwili sasa, na hivyo ukiukwaji wa haki za binadamu umetekelezwa.

Amnesty International inataka serikali ya khartoum kuwachukulia hatua maafisa hao wa usalama waliotumia nguvu kupita kiasi kuwakabili waandamannaji hao waliolalamikia kupandwa kwa maisha nchini humo.

Mwaka ulipita zaidi ya waandamanaji 180 waliuliwa kwa kupigwa risaisi jijini Khartoum.

Serikali ya Sudan imesema waandamanaji hao walikuwa wanahatarisha usalama wa raia wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.