Pata taarifa kuu
Rwanda-Kodi-uchumi-Sheria

Rwanda: mkurugenzi mkuu wa zamani wa hifadhi ya jamii atiwa nguvuni

Polisi nchini Rwanda imefahamisha kumkamata aliyekuwa mkurugenzi wa hifadhi ya jamii Angelique Kantengwa ambaye aliachiswa kazi mwanzoni mwa mwaka huu. Polisi inamtuhumu kosa la matumizi mabaya ya pesa za serikali.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akinyooshewa kidole kuwakandamiza wapinzani.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akinyooshewa kidole kuwakandamiza wapinzani. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Akizungungumza mbele ya bunge siku ya ijumaa juma lililopita, rais wa Rwanda Paul Kagame amesema inashangaza kuona wezi wa pesa za walipa kodi wanapotakiwa kuweka bayana matumizi ya pesa za serikali wanadai kuwa wananynayaswa kisiasa. Kagame amevitaka vyombo vya sheria kuwahukumu na pesa walisopora zirejeshwe. Hata hivyo rais Kagame hakutaja jina la mkurugernzi wa zamani wa kifahdi ya jamii.

Angélique Kantengwa ambaye kwa sehemu kubwa amekuwa akifany akazi katika banki na taasisi za kifedha za uma. Duru kutoka jijin Kigali zimearifu kuwa, Kabla ya kukamatwa kwake hakuna aliyefikiria kwamba anaweza kuhususishwa na kashfa hiyo. Polisi nchini Rwanda inasema inaendelea na uchunguzi huku akisalia korokoroni.

Mshauri wa zamani wa maswala ya uchumi wa rais Kagame, David Himbara aliekimbilia uhamishoni, anakituhumu chama tawala cha RPF ubadhirifu wa pesa za pensheni ya wanyarwanda. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, kiongozi huyo wa zmanai amekuwa akiikososa serikali ya raia Kagame kupitia mitandano ya kijamii kuhusika katika ubadhirifu wa fedha za hifadhi ya jamii na benki kuu ya Rwanda.

Kanali Tom Byabagamba na jenerali mstaafu Frank Rusagara ambao mmoja ni shemeji na mwingine ni kaka wa David Himabara wote walikamatwa wiki kadhaa zilizopita kwa tuhuma za kuchochea vurugu. Rwanda limekuwa taifa linalo sifika sana kutokanana na usimamizi wake mzuri wa fedha, jambo linalofanya wafadhili na wawekezaji kuwa na iamani sana na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.