Pata taarifa kuu
KENYA - SHERIA

Mahakama ya ICC yamtaka rais wa Kenya kuripoti mahakamani Octoba 8

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, wamemtaka rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufika mbele ya Mahakama hiyo tarehe 8 mwezi huu wakati wa kikao kuhusu kesi yake.

Uhuru Kenyatta akiwa Hege Kabla ya kuwa rais
Uhuru Kenyatta akiwa Hege Kabla ya kuwa rais
Matangazo ya kibiashara

Agizo hili linakuja baada ya Majaji hao kukataa ombi la mawakili wake, la kumtaka rais Kenyata kuhudhuria kikao hicho kupitia mkanda wa Video akiwa jijini Nairobi na pia wamekataa kuahirisha tarehe ya kikao hicho.

Ikiwa atakubali kwenda Hague, rais Kenyatta atakuwa rais wa kwanza aliye madarakani kufika mbele ya Mahakama hiyo.

Upande wa Mashtaka umekuwa ukiilaumu serikali ya Kenya kwa kukataa kushirikiana na Mahakama hiyo, na kupata ushahidi muhimu,kuhusu kesi yake ambayo imeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Kenyatta aliomba kikao hicho kuarihswa kwa sababu taraerhje nane atakuwa na mkutano kati ya Kenya, Uganda na Rwanda kuhusu miundo mbinu na tarehe 9 kuhusdhuria uhuru wa Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.