Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRCONGO-USALAMA

Burundi, jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waendelea kukanusha uwepo wa majeshi ya Burundi katika eneo la Kiliba

Serikali ya Burundi, Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) na serikali ya Kinshasa bado wanaendelea kukanusha uwepo wa majeshi ya Burundi mashariki mwa DRCongo katika bonde la Rusizi jimboni Kivu ya Kusini katika kitongoji cha Kiliba licha ya hivi karibuni idhaa ya RFI Kuthibitisha taarifa hii baada ya kufanya uchunhuzi na kushuhudia uwepo wa kambi ya jeshi la Burundi katika eneo hilo.

Mwanajeshi wa Burundi
Mwanajeshi wa Burundi Getty Images/ Bobby Model
Matangazo ya kibiashara

Eneo hilo la Kiliba ni karibu na mpaka wa Burundi na DRCongo, eneo linalo pakana na msitu wa Rukoko, maharufu sana kutokana na waasi wa makundi mbalimbali ya waasi wa Burundi na DRCongo kupiga kambi.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, yapo makubaliano ya siri baina ya serikali ya Kinshasa na Bujumbura kuruhusu jeshi la Burundi kufanya shughuli zao dhidi ya waasi wa Burundi walioko kwenye maeneo kadhaa ya DRCongo

Hata hivyo, tangu mwanzoni wa mwaka 2014, hapajawahi kuwa na operesheni ya pamoja ya aina yoyote kati ya majeshi ya Burundi na ya Congo ambapo waasi wa Burundi wa FNL wanaendesha harakati zao katika tarafa ya Uvira na ambapo askari hao wamekuwa wakishambuliwa mara kadhaa miezi ya hivi karibuni na waasi wa Burundi.

Aidha, uwepo wa askari wa FARDC unaripotiwa kuwa mdogo katika eneo la Kiliba na vitongoji vyake kadhaa na ambapo taarifa zinabaini uwepo wa kambi ya majeshi ya Burundi, huku vyamzo kadhaa vikithibitisha taarifa hii, na kuongeza kuwa, jeshi la Congo limepewa amri kutokukagua magari yoyote ya kijeshi ya Burundi.

Sanjari na hayo, askari wa Umoja wa Mataifa MONUSCO pia wanazuiliwa kufika katika baadhi ya maeneo hayo ambapo wananchi wanaamini kuwa licha ya vizuizi hivyo Umoja wa Mataifa na wataalam wake wangeweza kubaini kinachoendelea hapo kiliba mashariki ma DRC.

Hali hii imeendelea kuwatia wasiwasi wananchi wa maeneo hayo, ambao wanawashuhudia wanajeshi hao na shughuli zao za nenda rudi, lakini wanashangazwa na taarifa za serikali za Burundi na DRCongo kuendelea kukanusha, jambo ambalo limeendelea kuwatia hofu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.