Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA

Burkina Faso: kura ya maoni kuhusu kugombea kwa Compaoré

Serikali ya Burkina Faso imetangaza Jumannne Oktoba 21, kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya Katiba. Uamzi huo utapelekea rais Blaise Compaoré kugombea katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi Novemba mwaka 2015.

Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaoré.
Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaoré. RFI
Matangazo ya kibiashara

Rais Blaise Compaoré ametimiza miaka 27 akiwa madarakani, wakati ambapo Katiba ya nchi ya Burkina Faso haimruhusu kugombea kwa mara nyingine katika uchaguzi wa rais.

Baraza la mawaziri limekutana leo Jumanne Oktoba 21 ambapo limepitisha mswada wa sheria kuhusu marekebisho ya Katiba, mswada ambao utatumwa Bungeni kwa minajili ya kuitishwa kwa kura ya maoni.

“ Baraza la mawaziri limepitisha kwa pamoja mswada wa sheria kuhusu marekebisho ya Katiba ambao utatumwa Bungeni, kulingana na Ibara 163 ya Katiba kwa minajili ya kuitishwa kwa kura ya maoni", Baraza la mawaziri limetangaza.

Mswada huo iwapo utapitshwa, utamuwezesha rais Blaise Compaoré kuitisha kura ya maoni kulingana na Ibara ya 37 ya Katiba.

Kwa upande wake, kiongozi wa chama kimoja cha upinzani, Benewende Stanislas Sankara, amesema hashangazwi na jambo hilo.

" Baada ya kuonekana kuwa mazungumzo ya kisiasa yameshindikana, Tunaweza kusema kwamba kulikuwa na mpango wa siri uliyokua umeandaliwa na rais Blaise Compaoré", amesema Stanislas Sankara.

Chama tawala cha Blaise Compaoré kina wabunge 70, wakati ambapo kunahitajika kura 63 ili mswada huo upitishwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.