Pata taarifa kuu

Mali: msichana mdogo aliye ambukizwa virusi vya Ebola afariki

Vizara ya Afya ya Mali imethibitisha kifo cha msichana mdogo aliye ambukizwa virusi vya Ebola hivi karibuni. Mtoto huyo aliye kuwa na umri wa miaka miwili, alikua mtu wa kwanza kubainika na virusi vya Ebola katika aridhi ya Mali.

Wafanayakazi katika sekta ya afya wanamfanyia vipimo mtoto kwenye mpaka kati ya Guinea na Mali, Oktoba 2 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Wafanayakazi katika sekta ya afya wanamfanyia vipimo mtoto kwenye mpaka kati ya Guinea na Mali, Oktoba 2 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Mtoto huyo alibainika Ahamisi Oktoba 23 kuwa aliambukizwa virusi vya Ebola katika mji wa Kayes magharibi mwa Mali, na hali yake kuthibitishwa Ijumaa Oktoba 24.

“ Licha ya jitihada zilizofanywa na Idara za Afya, mtoto huyo hatimaye amefariki”. Hizo ni kauli ziliyo kua zikitumiwa na viongozi wa Mali. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa hospitali ya Kayes, mtoto huyo alifanyiwa vipimo Alhamisi Oktoba 23 na Ijumaa Oktoba 24, na hali yake ilikua ikiendelea vizuri.

Wazazi wa marehemu huyo ni wakaazi wa mji wa Kayes magharibi mwa Mali. Aliingia Mali akitokea Guinea. Awali viongozi wa Mali walisema kwamba watu waliyogusana au kuwa karibu na mtoto huyo waliwekwa karantini na tayari wamefanyiwa vipimo ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Msichana huyo alikua na homa na alikua akitokwa damu puani.

Wizara ya afya ya Mali imewataka raia kuwa na utulivu, na kubaini kwamba viongozi wanafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kuwa ugonjwa huo umedhibitiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.