Pata taarifa kuu
TANZANIA-POLISI-Sensa-Haki za binadamu-Usalama

Tanzania yaanzisha zoezi la kuwatambua raia wake

Idara ya Uhamiaji Tanzania ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM inatarajia kuandikisha raia wake wote ikianza na wale waishio mikoa ya mipakani magharibi mwa Tanzania ili kuboresha zaidi kumbukumbu za kiuhamiaji. 

Baadhi ya watoto waliyokua wakiishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mtabila mkoani Kigoma nchini Tanzania wakicheza ngoma ya asili ya taifa la Burundi
Baadhi ya watoto waliyokua wakiishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mtabila mkoani Kigoma nchini Tanzania wakicheza ngoma ya asili ya taifa la Burundi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Naibu kamishna wa Idara ya uhamiaji mkoani Kigoma, Embrosy Kingdom Mwanguku, amebaini kwamba serikali ya Tanzania itaandikisha raia wake kwa nchi nzima. Zoezi hilo litaanzia katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Gaita.

“ Lengo kuu la zoezi hili ni kuwezesha serikali kuboresha uwezo katika uendeshwaji wa maswala ya uhamiaji”, amesema Kingdom Mwanguku.

Kigoma ni miongoni mwa mikoa ambayo imekua ikipokea raia wa kigeni wanaoingia katika mkoa huo kinyume cha sheria. Wengi wa wahamiaji hao haramu ni kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.

Baadhi ya raia wa mkoa wa Kigoma wamesemna kuridhishwa na zoezi hilo, wakibaini kwamba zoezi lina manufaa makubwa ili kuweza kupata takwimu sahihi za wageni waliopo Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.