Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA-USALAMA-UCHAGUZI

Mgawanyiko wajitokeza katika chama cha rais wa zamani wa zambia

Vita vya kumrithi aliyekuwa rais wa Zambia, Michael sata, ambaye alifariki ghafla mwishoni mwa mwezi Oktoba vimeibuka. Mvutano umeendelea kushuhudiwa kati ya makundi mawili kutoka chama cha Patriotic Front, ukisalia tu mwezi mmoja na siku kadhaa ili uchaguzi wa urais ufanyike.

Hayati rais wa Zambia Michael Sata, ambaye chama chake kinakabiliwa na malumbano.
Hayati rais wa Zambia Michael Sata, ambaye chama chake kinakabiliwa na malumbano. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo unatazamiwa kufanyika Januari 20 mwaka 2015. Kila kundi linadai kukiwakilisha chama hicho.

Chama cha Patriotic Front kina wagombea wawili katika uchaguzi wa urais. Jumapili iliyopita wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho, Waziri wa sheria, Edgar Lungu, alichaguliwa kuwa mgombea wa chama cha Patriotic Front katika uchaguzi ujao. Ila kwa kuwa wafuasi wake tu ndio walikuwepo wakati wa uchaguzi, Edgar Lungu alipitishwa kwenye nafasi hiyo.

Siku moja baadae, kundi jingine kutoka chama hicho lilifanya mkutano na kumchagua Miles Sampa kama mgombea wa chama cha Patriotic Front kutoka kundi hilo. Sampa, mwenye umri wa miaka 44, anaungwa mkono na rais wa mpito wa sasa Guy Scott, ambaye hapaswi kugombea katika uchaguzi huo, kwani wazazi wake hawakuzaliwa Zambia.

Tangu kifo cha rais Sata, mvutano uliendelea kujitokeza kati ya Edgar Lungu na Guy Scott kuhusu kuhusu nani mwenye mamlaka ya uongozi wa chama. Kesi hiyo huenda ikafikishwa kwa mara nyingine mahakamani kutokana na wagombea wawili kwa tiketi ya chama kimoja.

Iwapo chama cha Patriotic Front kinashiriki uchaguzi wa januari 20 kikiwa kimegawanyika, itakua ni fursa kwa upinzani hususan rais wa zamani Rupiah Banda ambaye alitangaza hivi karibuni nia yake ya kugombea uchaguzi wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.