Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-NGESSAN-FPI-UCHAGUZI-SIASA

Mvutano wajitokeza katika chama cha FPI

Mvutano umeendelea kushuhudiwa katika chama cha FPI cha Laurent Gbagbo, nchini Côte d’Ivoire. Jumanne, Pascal Affi N'Guessan, mwenyekiti wa chama hicho cha upinzani, alitangaza kuwa mkutano wa chama kumchagua rais mpya huenda ukahirishwa.

Kaimu kiongozi wa chama cha FPI, Pascal Affi N'Guessan wakati wa sherehe za kutamatisha mkutano wa 8 wa chama chake, Abidjan, Februari 22 mwaka 2014.
Kaimu kiongozi wa chama cha FPI, Pascal Affi N'Guessan wakati wa sherehe za kutamatisha mkutano wa 8 wa chama chake, Abidjan, Februari 22 mwaka 2014. AFP/Issouf Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Lakini leo Jumatano Desemba 10, kumejitokeza hali ya kutoelewana, baada ya Sébastien Danon Djédjé, rais wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa chama ametangaza kuwa utafanyika kwa muda uliyopangwa.

“ Mkutano utafanyika Alhamisi Desemba 11kama ilivyopangwa”, amesema Sébastien Danon Djédjé.

“ Mkutano utafanyika, hata kama chama kimegawanyika katika makundi mawili ya wafuasi wanaomuunga mkono Laurent Gbagbo na wafuasi wa Affi N’Guessan. Kama mkutano hautofanyika kuna hatari vurugu katika chama ziendelea, na hali hiyo haiwezi kuonyesha sura nzuri. Muda imewadia wa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kutafutia ufumbuzi matatizo hayo”, ameendelea kusema Sébastien Danon Djédjé.

Hivi karibuni, kumeibuka na mgogoro mkubwa ndani ya chama ambapo kundi moja linamtaka aliyekuwa rais Gbagbo kugombea uenyekiti wa chama hicho, jambo ambalo linatupiliwa mbali na mwenyekiti anayemaliza muda wake Pascal Affi N'Guessan na ambaye ametangaza hatua ya kuahirishwa kwa mkutano kuepuka mpasuko ndani ya chama.

Mgawanyiko kati ya kamati kuu ya usimamizi wa chama na baadhi ya watendaji tayari umejidhihirisha hivi sasa katika chama hicho ambapo wengi bado wanaamini uhalali wa Gbagbo katika chama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.