Pata taarifa kuu
TUNISIA-Uchaguzi-Siasa

Uchaguzi wa urais Tunisia: kambi ya BCE yadai ushindi

Nchini Tunisia, matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais yanatarajiwa kutangazwa mapema Jumatatu Desemba 22. 

Beji Caïd Essebsi, baada ya kupiga kura mjini Tunis, Desemba 21 mwaka 2014.
Beji Caïd Essebsi, baada ya kupiga kura mjini Tunis, Desemba 21 mwaka 2014. REUTERS/Anis Mili
Matangazo ya kibiashara

Lakini chama cha Nidaa Tounes tayari kimetangaza ushindi wa mgombea wake Beji Caid Essebsi, bila kufafanua kura alizopata dhidi ya msindani wake, Moncef Marzouki, rais anaye maliza muda wake.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa Jumapili Desemba 21 kwenye saa 12 jioni saa za Tunisia.

Mohsen Marzouk aliye kuwa akisimamia kampeni ya Beji Caid Essebsi, alifanya mkutano na vyombo vya habari akieleza kuwa kulingana na uchunguzi walioendesha kuhusu matokeo ya uchaguzi, mgombea wa chama cha Nidaa Tounes ameshinda uchaguzi.

Narzouk amesema kuwa Caid Essebsi amemshinda kwa kishindo mshindani wake, bila hata hivyo kufafanua kura alizopata.

" Kwa mujibu wa viashiria ambavyo tunavyo, Mheshimiwa Beji Caid Essebsi ni mshindi wa uchaguzi wa rais. Nadhani kuna tofauti kubwa kati ya kura alizopata na alizopata mshindani wake. Tunamshukuru mshindani wetu bila shaka, mgombea Moncef Marzouki, kwa sababu ili kuwepo na demokrasia halisi ni lazima kuwepo na [wagombea] wawili", amesema Marzouk.

Mohsen Marzouk tayari ametangaza kuanza kazi hivi karibuni, huku akitoa kipaumbele kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Marzouk amewatolea wito wafuasi wa Beji Caid Essebsi kuelewa matokeo haya. Amewatolea wito pia kudumisha umoja wa kitaifa na kuahidi kushirikiana na wanasiasa wote ili kuendeleza gurudumu la siasa nchini Tunisia.

" Kila mtu anapaswa kuelewa kuwa ni lazima kuchukua matokeo haya kwa staha kubwa kwa sababu kibarua kinachotusubiri katika sekta ya maendeleo, uchumi na jamii ni muhimu sana'', amesema Marzouk.

Mpaka sasa matokeo rasmi hayajatangazwa, lakini baada ya tangazo lililotolewa na chama cha Nidaa Tounes, bendera za chama cha Nidaa Tounes zimewekwa hewani kwenye milingoti pamoja na picha ya Beji Caid Essebsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.