Pata taarifa kuu
LIBYA-MISRI-USALAMA

Wanamgambo wa kiislamu wawateka Wamisri 20 nchini Libya

Wanamgambo wa kiislamu wamewateka takribani wamisri 20 waumini wa dini ya kikristo waishio Libya kwa mujibu wa chanzo kimoja cha karibu na serikali.

rfi
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Ansar al-Sharia waliwateka kumi na watatu jumamosi katika mji wa pwani Sirte na wengine saba walitekwa siku chache zilizopita.

Utambulisho wa mateka hao Bado haujabainika isipokuwa ilifahamika kuwa ni waumini wa dini ya kikristo.

Maelfu ya wamisri wanafanya kazi nchini Libya hususan katik aidara za ujenzi na viwanda wamekuwa wakilengwa katika mashambulizi kipindi hiki taifa hilo likiendelea kupoteza usalama.

Mnamo mwezi February, mwaka jana maiti za wamisri saba ambao walikuwa wakristo zilipatikana na majeraha ya risasi jirani na jiji la pili kwa ukubwa Benghazi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.