Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UNICEF-HAKI ZANINADAMU-USALAMA

UNICEF yanyooshea kidole serikali ya Sudani Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya watoto (UNICEF) limesema kuwa linahofia kuwa, mamia ya wavulana walitekwa nyara na kundi la waasi linaloiunga mkono serikali ya rais Salva Kiir.

Watoto waliotumiwa katia vita  katika sherehe za kuwapokonya silaha na kuwarejesha katika maisha ya kiraia, Februari 10 mwaka 2015, katika mji wa Pibor, katika mkoa wa Jonglei, (Sudani Kusini), zoezi hili lilikua likisimamiwa na UNICEF.
Watoto waliotumiwa katia vita katika sherehe za kuwapokonya silaha na kuwarejesha katika maisha ya kiraia, Februari 10 mwaka 2015, katika mji wa Pibor, katika mkoa wa Jonglei, (Sudani Kusini), zoezi hili lilikua likisimamiwa na UNICEF. AFP PHOTO/Charles LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

UNICEF imebaini kuwa utekeaji huo ulifanyika katika jimbo la Upper Nile mwishoni mwa juma lililopita.

Serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaongozwa na Riek Machar wamekanusha kuhusika na utekaji wa watoto hao.

UNICEF imesema watoto 12,000 wametekwa nyara na kusajiliwa na vikosi vya serikali na waasi kupigana katika vita vionavyoendelea.

Afisa wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, Claire McKeever amesema shirika hilo limekuwa likijaribu kuiomba serikali kuwatafuta wavulana buila mafanikio.

UNICEF imesema vijana hao wamegawanywa katika makundi mawili. Baadhi wamepelekwa kwenye kambi ya mafunzo. Huku wengine wakipelekwa eneo la Melut pembezoni mwa White Nile iliyopo kaskazini mwa nchi. Baadhi ya watu katika eneo hilo la Melut wanasema wameona vijana wenye umri chini ya miaka kumi na mbili wakiwa wamebeba bunduki.

UNICEF imekua na wasiwasi kwamba huenda kuna uwezekano kua watoto hao wapo katika mchakato wa kupelekwa kupambana na waasi. Kwa upande wake, serikali imesema haina mamlaka juu ya wapiganaji waliowateka watoto hao.

Wiki mbili zilizopita, Unicef ililani kitendo cha kuwateka nyara watoto 89. Kitendo ambacho kilitekelezwa na kundi la watu wenye silaha ambao hawajafahamika.

Watoto 12,000 ndio wamesajiliwa katika jeshi na makundi ya waasi tangu Desemba mwaka 2013 nchini Sudani Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.