Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINIMAREKANI-CHINA-MAZUNGUMZ)

Mvutano waendelea katika mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yanaelezwa kuwa huenda yakachukua muda zaidi mpaka pande zinazokinza zikafikia suluhu.

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa kila upande unadhani kuwa upande mwingine unapendelewa na wasuluhishi wa mzozo huo ikiwemo muungano wa nchi za IGAD na Umoja wa Afrika.

Safari hii kwenye mazungumzo mapya Umoja wa mataifa, Marekani na Uchina zinaelezwa kuwa zitashiriki lakini tayari serikali inadai haitakubali nchi nyingine zishirikishwe katika mazungumzo hayo, hatua ambayo hata wachambuzi wa mambo wanaona kuna mvutano wa kimaslahi.

Kujiingiza kwa nchi ya China katika juhudi za kutaka kujaribu kumaliza hali ya machafuko nchini Sudan Kusini kunaelezwa kuwa huenda kukawa na ushawishi kwa pande zinazokinzana hasa wakati huu ambapo jumuiya ya kimataifa imetangaza kusimama kidete kushughulikia suala hili.

China ambayo ni mwekezaji mkubwa kwenye nchi ya Sudan Kusini hasa katika sekta ya mafuta, itashiriki kwenye mazungumzo ya safari hii kujaribu kuzishawishi pande zinazokinzana nchini humo kukubaliana kuunda Serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.