Pata taarifa kuu
UN-BURUNDI-SIASA-USALMA

UN yaitaka serikali ya Burundi kukomesha ukatili wa Imbonerakure

Kamishna mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu ukatili na mateso yanayotekelezwa na vijana wa chama tawala nchini Burundi Cndd-Fdd, Imbonerakure.

Nchini Burundi, Imbonerakure wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali vya ukatili dhidi ya raia.
Nchini Burundi, Imbonerakure wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali vya ukatili dhidi ya raia. RFI
Matangazo ya kibiashara

Zeil Ra'ad Al Hussein amewaita vijana hao kuwa ni wanamgambo, ambao wamekua wakitishia maisha ya raia, hususan wafuasi wa vyama vya upinzani, wanahabari, wanaharakati wa mashirika ya kiraia pamoja na wafuasi wa chama tawala ambao hawaungi mkono rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu.

Baada ya siku nne ya ziara yake nchini Burundi ambayo ni ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu alipoteuliwa mwezi Septemba mwaka 2014, raia huyo wa Jordan ameelezea kuwa nchi ya Burundi inaonekana kuingia kwenye njia ya " vurugu na vitisho ", huku wanamgambo wa chama tawala cha Cndd-Fdd wakitenda maovu bila kujali.

Zeil Ra'ad Al Hussein ameitaka serikali ya Burundi kufanya kilio chini ya uwezo wake ili kukomesha ukatili huo unaotekelezwa na wanamgambo wa chama tawala Imbonerakure dhidi ya wanahabri, wanaharakati wa mashirika ya kiraia, wafuasi wa vyama vya upinzani pamoja na wafuasi wa chama tawala ambao hawakubaliane na muhula wa tatu wa rais Nkurunziza.

Hayo yanajiri wakati mashirika ya kiraia nchini Burundi yameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiliomba kupitisha azimio linalolitaka jeshi la Burundi kuwapokonya silaha vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd, Imbonerakure pamoja na raia wengine wanaozimiliki kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.