Suala la ugaidi lawagawanya wabunge Kenya
Nchini Kenya, baadhi ya wabunge wanamshinikiza kiongozi wao bungeni Aden Duale kujiuzulu baada ya kusema kuwa kwa muda wa mwezi mmoja ujao atatoa orodha ya watu wanaoshirikiana na kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka Somalia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Wabunge hao wamesema, viongozi kutoka Kaskazini Mashariki mwa Kenya wanachukua muda mrefu kutoa majina hayo na kusisitiza kuwa Duale ajiuzulu wadhifa wake kabla ya kutoa majina hayo.
Hata hivyo, Duale amesema hatajiuzulu na kueleza kuwa wanasiasa kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo wanafanya bidii kuhakikisha kuwa wanapigana na ugaidi.
Wakati huo huo mjadala unaendelea nchini Kenya ikiwa vijana waliojiunga na kundi la Al Shabab nchini Somalia waliopewa siku 10 wajisalimishe na kusamehewa ikiwa itakuwa ni sahihi kusamehewa.
Baadhi ya wabunge nchini humo wmeasema ikiwa watajisalimisha wachukuliwe hatua huku viongozi wa Kiislamu wakitaka serikali kuongeza muda huo.