Pata taarifa kuu
BURUNDI-EAC-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Burundi: ujumbe wa Jumuiya ya EAC wawasili Bujumbura

Mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki wamewasili Jumatano wiki hii mjini Bujumbura, nchini Burundi, kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo akiwemo rais Pierre Nkurunziza.

Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, rais wa Rwanda, Paul Kagame (kushoto) na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni (kulia).
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, rais wa Rwanda, Paul Kagame (kushoto) na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni (kulia). Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa jumuia hiyo kutuma ujumbe wa ngazi ya mawaziri kwenda Bujumbura katika jitihada za kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo ambayo kwa miaka mingi imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mawaziri hao wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanafanya ziara hiyo mjini Bujumbura, wakati maandamnao ya raia yanaendelea kupamba moto wakipinga Pierre Nkurunziza kuwania muhula watatu wakisema ni kinyume na Katiba ya nchi hiyo pamoja na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha, ambao ni sheria mama ya nchini hiyo.

Hatua hiyo imekuja wakati ambapo viongozi wamekosolewa kwa kukaa kimya huku hali nchini Burundi ikizidi kuwa mbaya zaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure alikuwa nchini Tanzania Jumatatu wiki hii ambako alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.
Hata hivyo maandamano mjini Bujumbura yameendelea leo Jumatano kwa siku ya 10. waandamanaji wameapa kutositisha maandamano hayo mpaka Pierre Nkurunziza aachane na mpango wake wa kuwania muhula wa tatu.

Jumanne wiki hii Korti ya Katiba ilimruhusu Nkurunziza kuwania muhula watatu, siku moja kabla ya naibu mkuu wa Korti hiyo kuitoroka nchi, akibaini kwamba alifanyiwa vitisho vya kuuawa baada ya kupinga kutia saini kwenye uamzi wa Korti ya Katiba unaomruhusu Nkurunziza kuwania Muhula watatu. Sylvere Nimpagaritse alisema kuwa Pierre Nkurunziza hana haki ya kuwania muhula wa tatu kwani ni kinyume na Mktaba wa amani na maridhiano wa Arusha pamoja na Katiba ya nchi. Sylvere Nimpagaritse alisema majaji waliyokubaliana na uamzi huo walifanyiwa vitisho vya kuuawa na kukubali kutia saini zao kwenye waraka unaotoa uamzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.