Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Afrika Kusini: rufaa kwa kesi ya Oscar Pistorius Novemba

Nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius anatazamiwa kusikilizwa mahakamani mwezi Novemba. Mwanariadha huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela kwa kumuua pasipo kukusudia mpenzi wake mwezi Februari mwaka 2013.

Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela Septemba 12 mwaka 2014.
Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela Septemba 12 mwaka 2014. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Kesi yake itachunguzwa katika Mahakama ya rufaa, kwa ombi la Ofisi ya mashtaka ya Afrika Kusini, ambayo inataka Oscar Pistorius apewe adhabu kubwa.

Hakuna tarehe iliyopangwa kwa kesi hiyo kusikilizwa, lakini Mahakama kuu ya Afrika Kusini imebaini kwamba kesi ya Oscar Pistorius itasikilizwa mwezi Novemba. Oscar Pistorius alihukumiwa kwa kosa lililosababisha kifo baada ya kumpiga risasi mpenzi wake mwezi Februari katika siku ya wapendanao inayosheherekewa kila tarehe 14 Februari.

Pistorius alithibitisha mara kadhaa kwamba alipiga risasi hovyo kwenye mlango akidhani kuwa aliingiliwa na jambazi.

Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014.
Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014. REUTERS/Werner Beukes/Pool

Mwendesha mashtaka alikata rufaa, kwani anaamini kuwa Oscar Pistorius alimuua mpenzi wake kwa makusudi, na angelihukumiwa kwa kosa la kuua.

Kesi hiyo itachunguzwa kwa misingi ya masuala ya kisheria wala sio kwa misingi ya undani kesi. Swali ni kujua iwapo mwanariadha huyo alikua na nia ya kuua kwa kupiga risasi kwenye mlango wa choo, ambako alikua akijificha mpenzi wake, au majaji waliamua kwa Oscar Pistorius alitumia silaha yake kwa uzembe.

Mahakama hiyo itaamua kama majaji hawakusoma sheria jinsi ilivyo au kama Mahakama itaamua kama Oscar Pistorius alitekeleza kosa la mauaji, ambalo adhabu yake ni kufungwa jela kati ya miaka 15 hadi maisha jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.