Pata taarifa kuu
Sudan - AU

Bashir kushiriki mkutano wa AU Afrika Kusini

Radio ya taifa nchini Sudani imearifu kwamba rais wa Soudani Omar Hassan Al Bashir ambae anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa Kivita ya ICC atahudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika huko jijini  Johanesbourg nchini Afrika Kusini.

rais wa Sudan Umar Hassan Al Bashir
rais wa Sudan Umar Hassan Al Bashir REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Abdel Rafie al-Obeid, muandishi wa habari wa radio Omdurman ambae anasafiri na rais Bashir amesema wapo kwenye uwanja wa ndege jijini kharthoum tayari kwa safari ambapo rais Bashir atahudhuria kikao cha Jumapili na Jumatatu.

Tangu mwaka 2009, mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC ilitowa waranti mara mbili ya kukamatwa kwa rais Bashir kwa tuhuma za makosa ya kivita na ya kibinadamu yanayotekelezwa na majeshi yake huko Darfour magharibi mwa Sudan, na tangu hapo rais Bashir amepunguza safari zake nje ya nchi.

Hata hivyo Bashir amekuwa akisafiri hata kuelekea katika nchi zilizo saini mktaba wa Roma kuhusu uundwaji wa mahakama hiyo ambazo zilikubali kushirikiana na mahakama hiyo.

Afrika Kusini ilisaini mkataba huo wa Roma mwaka 1998

machafuko yanayoendelea huko Darfour, eneo kubwa la ukanda wa magharibu mwa Sudan yalianza tangu mwaka 2003 wakati waasi walianza kukabiliana na vikosi vya serikali katika kupinga kile walichodai ubaguzi dhidi ya watu weusi katika serikali ya rais Bashiri ilio na watu wengi waarabu.

Omar al Bashiri yupo madarakani tangu mwaka 1989 kupitia mapinduzi ya kijeshi. Umoja wa Mataifa unasema kwamba watu laki 3 wamepoteza maisha na wengine milioni 2.5 wameyatoroka ma kwao.

Bashir pia anatafutwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kupitia waranti iliotolewa mwaka 2010 kwa makosa ya mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfour.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.