Pata taarifa kuu
LIBYA-IS-MUJAHIDINI-MAPIGANO-USALAMA

Libya: Islamic State yatimuliwa Derna

Kwa karibu wiki mbili, mapigano makali katika mji wa Derna, nchini Libya, yameshuhudiwa kati ya wapiganaji wa kundi la Mujahideen, lenye mafungamano na Al-Qaeda, na wapiganaji wa kundi la Islamic State linaloendesha harakati zake nchini Libya, tangu Novemba mwaka 2014.

Bandari ya Derna, Libya.
Bandari ya Derna, Libya. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi Juni 20, mapigano yalisababisha vifo vya watu kadhaa pembezoni na katika mji wa Derna, kwa mujibu wa shirika la habari la Libya, Lana.

Mapigano kwa sasa yanaendelea kushuhudiwa nje kidogo ya mji wa Derna. Kundi la Islamic State liliudhibiti mji huo uliopo mashariki mwa Libya, na kuufanya ngome yake kuu. Lakini kwa wiki moja, kundi hili kutoka Iraq lilitimuliwa kutoka kituo chake na " Kundi la Mujahideen la Derna ", ambalo ni muungano ulioanzishwa na kundi la wafuasi wa Abu Salim na kuongozwa na maveterani wa Libya wa jihadi nchini Afghanistan.

Tangu kuonekana mwanzoni mwa mwaka 2014 wapiganaji wanaounga mkono kundi la Islamic State katika mji wa Derna, hususan raia wa kigeni kutoka Syria na Iraq, mji huo ulikumbwa na mauaji ya mara kwa mara. Mauaji ambayo yalionekana kuwa sugu, na kusababisha mvutano kati ya kundi hilo na mahasimu wa kundi la wafuasi wa Abu Salim. Kundi la Islamic State linawalaumu wapiganaji hao wa Abu Salim kwamba halikula kiapo cha kumtii kiongozi wao kutoka Iraq Al-Baghdadi, lakini pia kuwa karibu na wanamgambo wa Fajr Libya walio madarakani mjini Tripoli.

Tarehe 10 Juni, kundi la Islamic State lilimuua kiongozi wa kundi la Abu Salim na naibu wake, ambaye alikua mmoja wa maveterani wa al-Qaeda nchini Afghanistan. Mauaji hayo yalisababisha mapigano kuanza kati ya makundi hayo mawili. Baada ya vifo vya zaidi ya watu 20 na mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga, " Kundi la Mujahideen " lilizidhibiti ndani ya siku kumi ngome zote za Islamic State katikati ya mji wa Derna, ikiwa ni pamoja na makao makuu ya polisi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.