Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UN-UKATILI-HAKI

Sudan Kusini: UN yalaani ukatili wa kivita

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umetoa ripoti inayolaani ukatili unaotekelezwa katika machafuko ya kisiasa yanayochochewa kikabila ambayo yanaendelea kuiathiri ya Sudani Kusini kwa mwaka mmoja na nusu sasa.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inatumia ushahidi wa waathirika na mashahidi ambao walikimbia mapigano.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inatumia ushahidi wa waathirika na mashahidi ambao walikimbia mapigano. REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii inaonyesha jinsi gani haki za binadamu zimevunjwa katika mapigano yanayoendelea kushuhudiwa kati ya wanajeshi watiifu wa rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar. Machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu wengi. Watu milioni 2 wameyahama makaazi yao na takribani 300,000 wamekimbilia nchi jirani.

Wasichana na wanawake walibakwa na kisha kutupwa wakiwa hai katika nyumba zao zilizokua zikiteketea kwa moto, mauaji, utekaji nyara na vitendo vingine vya kikatili vimekua vikishuhudiwa nchini Sudan Kusini.

Ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana vimeendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo changa barani Afrika. Ripoti hii inaeleza kuwa si chini ya matukio tisa ya ukatili yaliyotekelezwa katika machafuko yanayoendelea nchini Sudan Kusini. Lakini pia utekaji nyara na mateso, kama vile kuchomwa mikono ili kuweza kusema maeneo gani wanakojificha waasi, au wanajeshi wa serikali.

Kwa kutoa ripoti hii, wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, walitumikia kwenye maelezo zaidi ya mia moja waliyopewa na watu waliotendewa ukatili huo pamoja na mashahidi wa jimbo la Unity, kaskazini mwa nchi hiyo. Wachunguzi wa Umoja wa Matifa walijaribu kuingia bila mafaniko katika maeneo kulikokuwa kukitekelezwa vitendo mbalimbali vya kikatili, kwani hawakuruhusiwa.

Umoja wa Mataifa unalituhumu jeshi la Sudan Kusini na waasi kuhusika na vitendo hivyo viovu katika mapigano makali yaliyozuka katika eneo hilo mwezi Aprili mwaka huu. Akihojiwa na RFI, msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, Philip Aguer, amethibitisha kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kujua waliohusika na ukatili huo.

" Kama ripoti inathibitisha kweli vitendo hivyo, wale ambao wametekeleza vitendo hivyo watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwa sababu ni uhalifu dhidi ya binadamu ", anasema Philip Aguer.

Wiki mbili zilizopita, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (Unicef) lilitoa ripoti inayozituhumu pande husika katika machafuko ya Sudan Kusini kuhusika na mauaji ya watoto, ubakaji, na vitendo vingine viovu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.