Pata taarifa kuu

Salva Kiir aapishwa kuendelea kuiongoza Sudan Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameapishwa kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka mitatu ijayo kutokana na mzozo unaoendelea.

Rais Salva Kiir, ameapishwa kuingoza Sudan Kusini kwa muda wa miaka mitatu ijayo.
Rais Salva Kiir, ameapishwa kuingoza Sudan Kusini kwa muda wa miaka mitatu ijayo. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wabunge jijini Juba baada ya kula kiapo hicho rais Kiir amesema ataendelea kufanya bidii kuleta amani nchini humo.

Wakati huo huo Sudan Kusini leo Alhamisi inaadhimisha miaka minne ya uhuru tangu ilipojitenga na Sudan mwaka 2011.

Maadhimisho haya yanafanyika wakati huu vita vikiendelea kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wanaoongozwa na Riek Machar kwa mwezi wa 18 sasa.

Maelfu ya wananchi wamepoteza maisha na wengine kuyahama makaazi yao.

Kutokana na mzozo huu, bunge lilimwongezea muda wa kuendelea kukaaa madarakani rais Slva Kiir kwa miaka mitatu zaidi na aliapishwa bungeni Jumatano wiki hii.

Riek Machar, kiiongozi wa waasi anayetaka Kiir na serikali yake kujiuzulu anasema kinachoendelea ni ukiukwaji wa katiba ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.