Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA

Rais Kikwete awatolea wito raia kuitikia uchaguzi wa mwezi Oktoba

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amewaambia wananchi wa taifa hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata nafasi ya kupiga kura wakati wa Uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete awotolea wito raia kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2015.
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete awotolea wito raia kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2015. TZ govt
Matangazo ya kibiashara

Akilihutubia bunge kwa mara ya mwisho wakati wa kulivunja mjini Dodoma, kiongozi huyo amesema kuwa serikali inaridhika na namna zoezi hilo linavyoendelea.

Wakati hayo yakijiri, wafuasi wa chama tawala CCM wanatarajiwa kufahamu mgombea wa chama hicho wakati wa uchaguzi wa urais mwishoni mwa juma hili.

Watu 38 walijitotokeza kuomba tiketi ya chama hicho na zeoezi la mchujo limekuwa likiendelea jijini Dodoma makao makuu ya chama hicho.

Halmashauri kuu ya chama inatazamiwa kukutana Ijumaa Julai 10 ambapo itachuja majina matano hadi kufikia matatu kupitia mtindo wa kupiga kura. Majina haya matatu ndiyo yatakayokwenda katika Mkutano mkuu wa Chama ambao ndio utakaochagua jina moja la mgombea urais kwa tiketi ya chama tawala cha CCM

Mkutano mkuu wa chama cha CCM unajumisha wanachama 2100 ikiwa ni pamoja na Wabunge wa CCM Tanzania bara na wawakilishi wengine kutoka Zanzibar lakini pia wawakilishi wa chama kutoka ngazi mbalimbali hadi ngazi za chini.

Hata hivyo mkutano huu mkuu wa chama cha CCM umepangwa kufanyika tarehe 11 hadi 12 Julai mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.