Pata taarifa kuu
KENYA-MGOMO-ELIMU

CORD yakerwa na mgomo wa waalimu Kenya

Muungano wa upinzani nchini Kenya CORD umewaambia viongozi wao katika Bunge la kitaifa na lile la Senate kuandaa mswada wa kukosa imani na rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta.

Raila Odinga, Waziri mkuu wa zamani, akiwa pia kiongozi wa upinzani,Julai 7, 2014 mjini Nairobi.
Raila Odinga, Waziri mkuu wa zamani, akiwa pia kiongozi wa upinzani,Julai 7, 2014 mjini Nairobi. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa upinzani wanasema wanachukua hatua hiyo kwa sababu rais Kenyatta ameshindwa kuiheshimu Katiba na kutii amri ya Mahakama ya kuitaka serikali kuwalipa walimu ili kumaliza mgomo unaoendelea.

Nacho chama wa walimu wa shule za sekondari kimemtumia barua Spika wa bunge la kitaifa kuitisha kikao cha dharura kujadili suala la mgomo huu wa walimu.

Serikali ya rais Uhuru Kenyatta inasema haina pesa za kuwaongezea walimu mshara, huku Wizara ya elimu ikisema mitihani ya kitaifa ya darasa la Nane na Kidato cha nne itaendelea kama ilivyopangwa, na uzinduzi wake utafabyika Ijumaa wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.