Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Usalama waendelea kudorora Mashariki mwa DRC

Mashirika ya kiraia wilayani Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo yamewataka wafanyabiashara pamoja na kampuni zisizo za kiserikali kutolipa kodi za serikali kama hatua ya kuishinikiza serikali kuimarisha usalama wa wananchi katika wilaya hiyo.

Wilayani Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo. Naibu mkuu wa majeshi ya MONUSCO, meja jenerali Jean Baillaud, akitembelea maeneo ya Oicha na Mbau kulikotokea.Mei 19, 2015.
Wilayani Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo. Naibu mkuu wa majeshi ya MONUSCO, meja jenerali Jean Baillaud, akitembelea maeneo ya Oicha na Mbau kulikotokea.Mei 19, 2015. MONUSCO/Myriam Asmani
Matangazo ya kibiashara

Katika mahajiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya RFI , mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu wilayani beni eneo lilishuhudia mauaji ya zaidi ya watu mia nane, wengi baadhi yao wakikatwa kwa mapanga, Jean paul Ngahangondi, amesema hatua hii imechukuliwa baada ya kushuhudiwa mauaji mengine mapya karibu na mji wa Oicha

Wabunge wa upinzani kutoka eneo hilo, wamesema kuwa hatua hii ni muhimu sana wakati huu, kukiwa na hali ya wasiwasi mjini Oicha na viunga vyake.

Hata hivyo Afisa wa Serikali ya Kinshasa aliyetumwa Mashariki mwa nchi hiyo kuhakikisha utawala wa serikali unaenea kwenye eneo hilo, Clovis Munihire, amesema kuwa hatua hiyo haina tija yoyote, amewataka wanaharakati hao kuungana na jeshi hilo, katika pambano dhidi ya waasi wa ADF, wanaosadikiwa kutekeleza mauaji ya wananchi.

Wilaya ya beni na viunga vyake imeendelea kushuhudiwa mauaji raia, huku makundi ya watu wenye silaha, hususan waasi wa Uganda wa ADF wanaoendesha harakati zao Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakiendelea kunyooshewa kidole kuhusika na mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.