Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Matokeo ya uchaguzi yaanza kutangazwa Tanzania

Matokeo ya awali kuhusiana na Uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili Oktoba 25 yameanza kutolewa leo Jumatatu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ya kiashiria Mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli anaongoza kwa wingi wa kura angalau kwa hivi sasa dhidi ya Edward Lowassa wa Chadema.

Zoezi la uhesabuji wa kura limeanza shughuli katika kituo kimojacha kupigia kura Dar es Salaam, Oktoba 25, 2015.
Zoezi la uhesabuji wa kura limeanza shughuli katika kituo kimojacha kupigia kura Dar es Salaam, Oktoba 25, 2015. AFP/DANIEL HAYDUK
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Tume waliojifungia katika jengo la jumba la mikutano la Julius Nyerere, mjini Dar es salaam wanaendelea kutangaza matokeo hayo ya Uchaguzi japo kwa mwendo wa kinyonga na hadi alasiri majira ya Afrika Mashariki, kiasi matokeo ya Majimbo matatu yalikuwa yamekwishatangazwa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeendelea jioni hii kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 13 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli anaongoza kwa majimbo tisa wakati mgombea wa CHADEMA, Edward Lowasa akiongoza majimbo manne.

Mapema Asubuhi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, jaji Mstaafu Damian Lubuva alitangaza majimbo matatu ambayo ni Paje, Makunduchi, na Lulindi ambayo yote Magufuli aameongoza.

Waziri wa sasa wa Ujenzi, John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),katika kampeni ya uchaguzi jijini Dar es Salaam Oktoba 23.
Waziri wa sasa wa Ujenzi, John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),katika kampeni ya uchaguzi jijini Dar es Salaam Oktoba 23. REUTERS/Sadi Said

Majira ya alaasiri Jaji Lubuva alitanga majimbo mengine 10 ambapo kati ya hayo Magufuli anaongoza katika majimbo sita ikiwa ni pamoja na Ndanda , Nsimbo, Kibaha,, Bumbuli, Donge, na Kiwengwa.

Naye Edward Lowasa aliongoza katika majimbo manne ambayo ni Kiwani, Chambani, Mtambile na Mkoani.

Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu na mgombea wa chama cha upinzani cha Chadema (katikati) wakati wa kampeni za uchaguzi katika Wilaya ya Kilosa katika Mkoa wa Morogoro, Oktoba 23, 2015.
Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu na mgombea wa chama cha upinzani cha Chadema (katikati) wakati wa kampeni za uchaguzi katika Wilaya ya Kilosa katika Mkoa wa Morogoro, Oktoba 23, 2015. REUTERS/Stringer

Tume ya Uchaguzi imeweka hakikisho kwamba zoezi hilo litakamilika kabla ya oktoba 29 ambapo wanatumai Rais mteule atatangazwa mapema mwishoni mwa juma hili.

Wakati huo huo Mgombea wa CHADEMA chini ya Muungano wa upinzani nchini Tanzania UKAWA, Edward Lowassa, ameikosoa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kutangulia kimkakati kutangaza matokeo katika maeneo ambayo mgombea wa CCM anaongoza kwa wingi wa kura.

Hayo yakijiri Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania CCM kimeshtumu hatua ya chama cha upinzani cha CUF kutangaza matokeo na kudai ushindi ikisema ni ya kushangaza.

CCM imesema kuwa matangazo hayo ni kinyume na sheria kwa kuwa bodi pekee inayofaa kutangaza matokeo ni ile ya tume ya uchaguzi.

Kwa upande wake Mkuu wa tume ya uchaguzi jaji Damian Lubuva ameonya kwamba ni matokeo ya tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC pekee ambayo yatakuwa rasmi na hakuna aliye na uwezo wa kuyatangaza matokeo yake hata iwapo wameshinda.

Muungano wa upinzani nchini Tanzania UKAWA umedai kwamba vijana wake 200 ambao waliokuwa wakikagua matokeo yanayotolewa kutoka kwa maajenti wake katika vituo vya kupiga kura kote nchini walikamatwa usiku uliopita na sasa wako kizuizini.

Naibu mwenyekiti wa muungano huo Profesa Abdalla Safari amesema kuwa vijana hao walikamatwa wakati maafisa wa polisi walipovamia vituo vya uchaguzi vya upinzani na kuchukua data muhimu na kompyuta.

Muungano huo umedai kwamba hatua hiyo ya maafisa wa polisi itawalazimu kupinga matokeo yoyote yatakayotolewa na tume ya uchaguzi NEC, ukisema kuwa umewachwa bila ushahidi wa kuonyesha kwamba kuna udanganyifu katika matokeo ya uchaguzi.

UKAWA imesema kuwa hautakubali matokeo hayo huku profesa Simba akisema kuwa uwezo wa raia utaamua mwelekeo wa taifa iwapo matokeo hayo hayatawapendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.