Pata taarifa kuu
DRC-UN-BAN-WAKIMBIZI

DRC: Ban Ki-moon akutana na wakimbizi kutoka kambi ya Kitchanga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewasili Jumanne hii jioni nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ban atakutana Jumatano hii Februari 24 na Rais Joseph Kabila, upinzani na vyama vinavyoiunga serikali mkono kwa kujaribu kupata ufumbuzi wa kile kinachoendelea kuonekana kuwa mgogoro wa kisiasa.

Na Ki-moon katika kambi ya Kitchanga, Kivu Kaskazini, Februari 23, 2016.
Na Ki-moon katika kambi ya Kitchanga, Kivu Kaskazini, Februari 23, 2016. © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo matarajio ya uchaguzi wa rais ambao tarehe iliopangwa kikatiba imepuuziwa.

Ban Ki-moon, Jumanne hii, alikuwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo alitembelea kwa haraka kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa Kitchanga.

Katika kambi hiyo ya Kitchanga, Ban aliweza kukutana hasa na wanawake na watoto. Aliweza kuzungumza na wakimbizi hao wa ndani, licha ya kuwa muda wake uliku mfinyu sasa.

Wanawake wengi waliokimbilia katika kambia hiyo walimuelezez Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa masaibu yanayowakuta wanapojaribu kurudi katika makazi yao. Baadhi wameelezea vitisho vya kubakwa vinavyowakabili wanapojaribu kuondpka katika kambi hiyo.

Wanawake wamemueleza Ban kwamba wanataka kurudi nyumbani, lakini hakuna usalama. Wamemuomba Ban Ki-moon kusaidia kurejesha amani mashariki mwa DRC.

"Siku moja munaweza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa"

Hatua ya tatu katika kambi hiyo, Ban ameweza kukutana na watoto katika majengo ya shule yaliojengwa katika kambi ya Kitchanga. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaelezea watoto kwamba yeye mwenyewe alilazimika kukimbia akiwa mtoto wakati wa vita vya Korea. Na kwamba, kama wao, aliweza kusaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yalimsaidia kuishi na kumhudumia kielimu. "Inabidi mtumike kwa nguvu," Ban Ki-moon amewasihi. "Na siku moja, huenda pia mmoja wenu akawa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa au rais wa nchi hii."

"Leo tuna watu milioni 60 duniani kote. Hii ni idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani na wale wanaozikimbia nchi zao tangu mwisho wa vita vya Korea, amesema. Tunajaribu kufanya kilio chini ya uwezo wetu. Najua kwamba tunakabiliwa na ukosefu wa uwezo. Umoja wa Mataifa hauwezi kukabiliana peke yake. Hakuna nchi ambayo inaweza kufanya jambo hili peke yake. Tunahitaji msaada wa nchi wanachama. Kwa maana hiyo ntaitisha Mkutano wa wa kwanza utakaojumuisha nchi zote duniani, ambao utakua mkutano wa Historia juu ya hatua ya kibinadamu na kisha mwingine mwezi Septemba juu ya suala la uhamiaji na wakimbizi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.