Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-KASHFA-ZUMA-UCHUNI

Afrika Kusini: Jacob Zuma alengwa na utaratibu mpya

Bunge la Afrika Kusini litajadili pendekezo jipya la lawama dhidi ya Jacob Zuma. Waraka huu uliwasilishwa na upinzani, kufuatia uamuzi wa Mahakama ya kikatiba ambayo ilitoa uamuzi Alhamisi iliyopita.

Jacob Zuma, Machi 17, mbele ya Bunge la Afrika Kusini.
Jacob Zuma, Machi 17, mbele ya Bunge la Afrika Kusini. © DAVID HARRISON / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kikatiba ilibaini kwamba Rais wa Afrika Kusini amevunja Katiba kwa kukataa mpaka sasa kulipa sehemu ya fedha za umma zilizotumiwa kwa kukarabati makazi yake binafsi.

Huu ni utaratibu mwengine wa kung'olewa mamlaka unaokabili Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Maandamano dhidi yake ya hivi karibuni hayakuwa na nguvu. Tangu Alhamisi, Machi 30, wito wa kujiuzulu umeongezeka ikiwa ni pamoja na katika upande wa chama chake.

Maveterani kadhaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi wametoka katika ukimyaili kumuomba Rais Zuma kujiuzulu kufuatia uamuzi wa Mahakama ya kikatiba ambayo ilitoa uamuzi kuwa hatua ya Rais Zuma ni kinyume na katiba katika kusimamia kashfa ya Nkandla.

Hata hivyo hakuna bahati kwamba nafasi utaratibu huu utapitishwa Bungeni. Kunahitajika kura ya theluthi mbili ya Bunge. Licha ya kuwa chama cha ANC kina Wabunge wengi lakini hasa chama cha Jacob Zuma kimezuia mambo mengi dhidi ya rais wake.

Katika uamuzi wake, Mahakama ya kikatiba pia imewashtumu wabunge kwamba walishindwa kuwajibika katika majukumu yao kwa kutouliza shughuli za rais, hasa ukarabati wa makazi binafsi ya rais Zuma katika kijiji cha Kandla.

Kura ya Jumanne hii Aprili 5 inapaswa kuwa ya muhimu. Wabunge wa chama cha ANC wataonyesha kama kweli wanaeshimu Katiba, au wataendelea kuwa na imani na rais wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.