Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ICC

ICC yasikitishwa na uamuzi wa Afrika kusini na Burundi

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC jana Jumamosi imeziomba nchi za Afrika Kusini na Burundi kufikiria upya uamuzi wao wa kuondoka katika mahakama hiyo iliyoundwa kwa lengo la shughulikia kesi za uhalifu mkubwa zaidi ulimwenguni.

Fatou  Bensouda mwendesha mashitaka katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC
Fatou Bensouda mwendesha mashitaka katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC DR
Matangazo ya kibiashara

Rais wa mkutano wa vyama vya nchi wanachama waanzilishi wa mkataba wa ICC Sidiki Kaba amesema kuwa Ingawa kujiondoa kutoka katika mkataba huo ni kitendo huru,lakini anasikitika kwa maamuzi hayo na anaziomba Afrika Kusini na Burundi kufikiria upya maamuzi yao.

Aidha amezitaka nchi hizo kufanya kazi pamoja na mataifa mengine katika mapambano dhidi ya ukatili, ambao mara nyingi husababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kauli hii imekuja siku moja baada Afrika Kusini kuweka pigo kubwa kwa mahakama hiyo kwa kutangaza ikuwa inafanya mchakato wa kujiondoa kutoka ICC baada ya Burundi.

Afrika kusini imechukua uamuzi wa kuanzisha mchakato huo kufuatia kukumbwa na shinikizo mwaka uliopita kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.