Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-AFYA

Hali ya afya ya rais wa Zimbabwe yazua mijadala

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe yuko nchini Singapore kwa uchunguzi wa afya huku maofisa wa serikali wakikanusha taarifa za kiongozi huyo kuzidiwa, vyombo vya serikali nchini humo vimethibitisha.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati wa mkutano na maveterani wa vita vya ukombozi Aprili 7 mjini Harare.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati wa mkutano na maveterani wa vita vya ukombozi Aprili 7 mjini Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Sunday Mail limeandika kuwa rais Mugabe aliondoka nchini humo Ijumaa ya wiki iliyopita kuelekea nchini Singapore kwa matibabu na kwamba kiongozi huyo anatarajiwa kurejea katikati ya wiki hii.

Safari za rais Mugabe nchini Singapore zimeongezeka kwenye miaka ya hivi karibuni ambapo mara ya mwisho kuwa nchini humo ilikuwa ni mwezi Mei ambapo pia alisafiri kwa sababu za kimatibabu na mwaka 2011 na 2014 alifanyiwa operesheni ya jicho.

Afya ya rais Mugabe imeendelea kuzua mijadala nchini mwake ambapo mwezi Machi mwaka huu mamlaka nchini humo ziliwakamata waandishi wa habari wawili walioandika kuwa afya ya kiongozi huyo imezorota.

Licha ya umri alionao, chama chake cha ZANU-PF mwaka jana kilimteua kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao, huku kukiripotiwa mgawanyiko ndani ya chama hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.