Pata taarifa kuu
MISRI-SIASA

Mkuu wa zamani wa majeshi akamatwa Misri

Mkuu wa zamani wa majeshi ya Misri Sami Anan, ambaye chama chake kilimtangaza wiki mbili zilizopita kupeperusha bendera yake katika uchaguzi wa urais wa mwezi Machi.

Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Misri, Sami Anan.
Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Misri, Sami Anan. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Bw Anan ameamua kusitisha kampeni yake ya uchaguzi. Angelichuana na rais anayemalizi muda wake Abdel Fattah al Sissi Sama Anan amekamatwa leo Jumanne mjini Cairo, timu yake ya kampeni imetangaza.

Kukamatwa kwake kunakuja muda mfupi baada ya ttelevisheni yaserikali kupitisha taarifa ya jeshi inayotangaza kwamba Sami Anan anatafutwa kwa kuchochea mgawanyiko kati ya jeshi na raia pamoja na kughushi stakabadhi za serikali.

Sami Anan anashutumiwa kughushi hati ambayo inasema kuwa hana tena uhusiano na jeshi, moja ya masharti yanayohitajika ili kuwania kiti cha urais nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, kuwania kwa Sami Anan kunakiuka sheria na kanuni za jeshi kwa sababu angelitangaza hivyo "bila kupata idhini kutoka kwa jeshi (...) na bila kuchukua hatua za kuacha moja kwa moja shughuli zake za kijeshi ".

Jeshi halijesema lolote kuhusu kukamatwa kwa Bw Anan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.