Pata taarifa kuu
UFARANSA-TUNISIA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Rais wa Ufaransa azuru Tunisia

Baada ya ziara yake Novemba mwaka jana, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anafanya ziara nyingine katika bara la Afrika. Kabla ya Senegal mwishoni mwa wiki hii, atakuwa Tunisia leo Jumatano na kesho Alhamisi.

RAis Emmanuel Macron akiambatana na washauri wake katika masuala ya AfrikaAgosti 29, 2017, Élysée.
RAis Emmanuel Macron akiambatana na washauri wake katika masuala ya AfrikaAgosti 29, 2017, Élysée. REUTERS/Yoan Valat/Pool
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara yake ya kwanza nchini Tumisia tangu uchaguzi wa urais wa nchini Ufaransa. Ziara ya Rais Macron nchini Tunisia inakuja wakati ambapo nchi hiyo inaendelea kukabilia na mgogoro wa kisiasa.

Baada ya "kuzuru" Morocco, ziara ya "urafiki na kazi" nchini Algeria, Rais Macron sasa anazuru Tunisia kwa ziara ya serikali. Ziara ya kwanza ya Emmanuel Macron katika ulimwengu wa Kiarabu, Ikulu ya Elysée imesema.

Ziara ya Rais Macron nchini Tunisia ni moja ya njia ya kutuma "ujumbe mkali kusaidia" kuinua demokrasia nchini Tunisia. Kwa sababu, kwa upande wa ikulu ya Elysée, "kukabidhiana madaraka ni moja ya njia zilizofanikisha kukuwa kwa kidemokrasia baada mabadiliko yaliyotokea katika nchi za Kiarabu". Rais Emmanuel Macron atalihutubia Bunge la Tunisia kesho Alhamisi.

Wiki mbili baada ya maandamano yaliyoikumba Tunisia, masuala ya kiuchumi na kijamii yatakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo na Rais Beji Caib Essebsi. Matarajio ni mengi upande wa Tunisia, ambapo Ufaransa ndiye mshirika wake mkuu wa kwanza wa kiuchumi.

Sekta ya utalii nchini Tunisia bado inakabiliwa na athari ya mashambulizi ya mwaka 2015. Na ni vigumu nchi hiyo kujaribu kuwashawishi tena watalii kutoka Ufaransa kuingia nchini humo kwa mambo ya utalii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.