Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-USALAMA

Paul Biya kuapishwa kama rais wa Cameroon

Rais mteule wa Cameroon, Paul Biya, anatarajiwa kuapishwa leo kuendeleza kuongoza taifa hilo la Afrika ya Kati kwa muhula mwingine wa miaka saba.

Rais wa Cameroon Paul Biya.
Rais wa Cameroon Paul Biya. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Biya ataapishwa mbele ya wabunge jijini Yaounde, baada ya kutangazwa mwezi uliopita kushinda Uchaguzi wa urais, licha ya matokeo hayo kukataliwa na wagombea wa upinzani.

Biya mwenye umri wa miaka 85, amekuwa madarakani sasa kwa miaka 36.

Miongoni mwa mataifa ambayo yamempongeza rais Biya ni pamoja na China, Ufaransa na Senegal.

Paul Biya alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa marudio nchini Cameroon na hivyo kumfanya kuwa rais kwa mihula saba mfululizo.

Akiwa na miaka 85, Biya ndio rais mwenye umri mkubwa zaidi kusini mwa jangwa la Sahara na ushindi huo ulimfanya awe mmoja wa marais wa Afrika waliohudumu kwa muda mrefu zaidi. Raia wengi wa Cameroon wamemfahamu yeye tu kama rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.