Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-USALAMA

Paul Biya kutawazwa katika hali ya mvutano Cameroon

Rais wa Cameroon Paul Biya, mwenye umri wa miaka 85, ambaye yupo madarakani kwa muda wa miaka 36, anatarajiwa kutawazwa Jumanne wiki hii kwa muhula wa saba mfululizo.

Rais wa cameroon Paul Biya.
Rais wa cameroon Paul Biya. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Bw Biya anatawazwa katika hali ya mvutano kufuatia utekaji nyara wa wanafunzi 79 katika eneo linalozungumza Kiingereza linaloendelea kukumbwa na machafuko.

"Rais aliyechaguliwa" nchini Cameroon, Paul Biya, atatawazwa leo Jumanne saa 11:00 mchana (sawa na saa10:00 mchana saa kimataifa), ofisi ya rais imetangaza katika taarifa yake.

Meya wa mji wa Yaoundé amewatolea wito wakazi wa mji huo kuja kwa wingi kumuunga mkono rais Paul Biya kwa kazi kubwa ambayo anatarajia kufanya kwa muhula mwengine.

Sherehe za kutawazwa zitafanyika katika jengo la Bunge.

Sherehe hizi zinafanyika siku moja baada ya watu 82, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 79, walitekwa nyara na watu wenye silaha wasiojulikana katika mji wa Bamenda, mji mkuu wa kaskazini magharibi mwa Jimbo linalozungumza Kiingereza. Watu waliojihami kwa silaha walivamia shule ya Presbyterian Secondary School, inayomilikiwa na kanisa la Kiprotestanti.

"Zoezi la kuwatafuta mateka limezinduliwa," kwa mujibu wa chanzo cha serikali.

Katika video ya daikika sita, vijana kumi na moja wenye umri wa miaka kumi na tano, mmoja baada ya mwengine, wamejitambulisha kwa Kiingereza, na kusema wametekwa nyara na kundi la "Amba Boys", wanaharakati kutoka Jimbo linalozungumza Kiingereza ambao wanataka Jimbo lao kuwa taifa huru.

"Tutaanzisha shule zetu binafsi hapa, tutaishi pamoja na kupigania" Ambazonia ", taifa ambalo wanaharakati hao wanaotarajia kuunda, amesema mmoja wa watekaji nyara aliyejificha uso", kwa mujibu wa shirika la Habari la AFP.

Katika mkoa huo wa Kaskazini-Magharibi, naibu mkuu wa wilaya ya Noni pia alitekwa nyara siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.