Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA-HAKI

Rais wa Misri azindua Kanisa Kuu la Coptic

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi amezindua Kanisa Kuu la dhehebu la Coptic, Mashariki mwa Cairo, mji mkuu wa nchi hiyo. Hili ndio Kanisa kubwa la Coptic katika eneo la Mashariki ya kati.

Rais wa Misri Abdel Fattah al Sissi na Kiongozi wa Kanisa la Coptic Tawadros II wakati wa uzinduzi wa Kanisa Kuu la Coptic karibu na Cairo, Januari 6, 2019.
Rais wa Misri Abdel Fattah al Sissi na Kiongozi wa Kanisa la Coptic Tawadros II wakati wa uzinduzi wa Kanisa Kuu la Coptic karibu na Cairo, Januari 6, 2019. MOHAMED EL-SHAHED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uzinduzi huu umekuja, baada ya polisi mmoja kupoteza maisha wakati akiharibu bomu lililokuwa limetegwa juu ya Kanisa la Coptic nje kidogo ya jiji la Cairo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Polisi wengine wawili pia walijeruhiwa katika mlipuko huo wa bomulililokuwa katika mfuko, kwa mujibu wa vyanzo hivyo.

Rais Al Sisi amesisitiza kuwa ataendelea kuhakikisha kuwa waumiani wa Coptic ambao ni asilimia 10 ya raia wa nchi hiyo wanalindwa.

Kanisa la Coptic nchini Misri linaendelea kukumbwa na mashambulizi ya kundi la Islamic State (IS)tangu mwaka 2016. Kundi hili limedai kuhusika na mashambulizi kadhaa yaliosababisha vifo vingi dhidi ya jamii hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.