Pata taarifa kuu
HRW-MISRI

HRW: Serikali na wanajihadi wa kiislamu wanatekeleza uhalifu dhidi ya binadamu Sinai

Watetezi wa haki za binadamu wanasema kuwa vikosi vya Serikali ya Misri pamoja wanajihadi wa kiislamu kwenye eneo la Sinai, wote kwa pamoja wanawajibika kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Polisi na wanajeshi wa Misri wakipiga doria kwenye eneo la Sinai.
Polisi na wanajeshi wa Misri wakipiga doria kwenye eneo la Sinai. Khaled DESOUKI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Human Rights Watch linaituhumu Serikali kwa kutekeleza uhalifu ikiwemo utekaji, mauaji, mateso na makosa mengine ambayo ni kinyume cha sheria.

Shirika hilo linasema wanajihadi wa kiislamu ambao Serikali inakabiliana nao wamekuwa wakiwateka watu, wakiwatesa na kuua mamia ya raia wanaoishi kwenye eneo la Sinai.

Pande hizi mbili kwa muda mrefu sasa zimekuwa zikipigana kaskazini mwa rasi ya Sinai.

Serikali ya Misri ilitangaza eneo hilo la kaskazini kama eneo la operesheni za kijeshi, ikimaanisha kuwa eneo hilo haliko wazi kwa uripotiji habari huru ambapo iliahidi kuhakikisha inayamaliza makundi ya kijihadi yaliyoko kwenye eneo hilo, ambayo baadhi yanashirikiana na Islamic State.

Kwa mujibu wa ripoti ya Human Rights Watch, watu wazima na watoto walio na umri wa chini ya miaka 12 wamekuwa wakizuiliwa na kuhifadhiwa kwenye jela za siri na wakati mwingine kwa miezi kadhaa.

Human Rights Watch imeorodhesha nyaraka ambazo zinaeleza namna wahanga wa vitendo hivyo wamekuwa wakifanyiwa ikiwemo kupigwa kwa shoti ya umeme.

Ripoti inasema watatu kati ya waliowahi kukamatwa walipoteza maisha, ripoti hii imenukuu baadhi ya manusura.

Ripoti inasema tangu kuzuka kwa machafuko kwenye eneo hilo mwaka 2013, maelfu ya wakazi wamelazimika kukimbia nyumba zao huku wengine wakikimbia mapigano.

Human Rights inaituhumu pia Serikali kwa kutekeleza mashambulizi ya anga na ardhini kinyume cha sheria ambapo mamia ya watu wameripotiwa kupoteza maisha.

Shirika hili linawatuhumu wanajihadi wa kiislamu kwenye eneo la Sinai kwa kutekeleza makosa ya jinai ikiwemo utekaji, mateso na mauaji ya mamia ya wakazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.