Pata taarifa kuu
DRC-UBELGIJI

Mwili wa Tshisekedi kuondoka Ubelgiji Alhamisi hii

Safari ya kuurejesha mwili wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa DRC na kinara wa upinzani Etienne Tshisekedi, ambao bado uko nchini Ubelgiji, imeahirishwa katika dakika za mwisho hapo jana, watu wa karibu na familia wamethibitisha.

Jeneza la Etienne Tshisekedi, ambaye mwili wake umekuwa Brussels tangu afariki mwaka 2017
Jeneza la Etienne Tshisekedi, ambaye mwili wake umekuwa Brussels tangu afariki mwaka 2017 REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema kuwa safari hiyo iliahirishwa kutokana na sababu za masuala ya usafiri wa ndege, ambapo watu zaidi ya 250 walikuwa wamepanga kuusindikiza mwili wake hadi jijini Kinshasa.

Ubelgiji ilikuwa imepanga kufanya gwaride la kijeshi kama heshima kwa kiongozi huyo wa zamani wa DRC, ambapo waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders alikuwa ahudhurie.

Tshisekedi ambaye mtoto wake Felix aliapishwa mwaka huu kuwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwili wake umekuwa ukisubiriwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Tangu Tshisekedi afariki dunia wakati wa utawala wa Joseph Kabila, familia ya Tshisekedi ilikuwa ikivutana na Serikali wakati huo kuhusu mahali ambapo mwili wake utazikwa hali iliyosababishwa kushelewesha kuurejesha mwili wake.

Mwili huo sasa utasafirishwa Alhamisi ya wiki hii kuelekea DRC tayari kwa mazinshi yaliyopangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili.

Tshisekedi alifariki dunia akiwa mjini Brussels mwezi February mwaka 2017.

Kwa miongo kadhaa Etienne Tshisekedi alikuwa akifanya harakati za kisiasa kama kiongozi wa upinzani lakini hakuwahi kushika nafasi hiyo ya juu mpaka anafariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.