Pata taarifa kuu
GAMBIA-JAMMEH-SIASA-USALAMA

Gambia: Yahya Jammeh atakamatwa iwapo atarejea nchini

Serikali ya Gambia kupitia waziri wa sheria, imeonya kuwa rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh atakamatwa iwapo atajaribu kurejea nchini humo.

Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh (kulia) na mshirika wake wa karibu, Edward Singhateh, afisa wa zamani wa jeshi la Gambia, hapa ilikuwa maaka 2006.
Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh (kulia) na mshirika wake wa karibu, Edward Singhateh, afisa wa zamani wa jeshi la Gambia, hapa ilikuwa maaka 2006. Seyllou Diallo/AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Sheria Aboubacarr Tambadou, amesema Yahya Jammeh, ambaye anayeshi nchini Equatorial Guinea tangu mwaka 2017 atafunguliwa mashtaka kuhusu masuala mbalimbali wakati wa uongozi wake.

“Iwapo rais wa zamani wa Yahya Jammeh atarudi hapa nchini, atakakamtwa na kushtakiwa. Atawajibishwa kama mtu wa kawaida hapa nchini, kutakuwa na uwajibikaji mkubwa, nawahakikishia waathiriwa wa makosa haya, “ amesema waziri wa sheria wa Gambia.

Hivi karibunui, Jammeh amekuwa akisema anatamani kurudi nyumbani, huku wafuasi wake wakionya kuwa akikamatwa, kitendo hicho kitasabisha umwagaji damu katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi.

Yahya Jammeh, ambaye alitawala kwa mkono wa chuma kwa miaka 22 na ambaye anaendelea kuishi uhamishoni kwa miaka mitatu sasa, nchini Equatorial Guinea, alisikika hivi karibuni nchini Gambia kupitia sauti iliyorekodiwa kwa simu, ambapo anabaini kwamba anatamani kurudi nchini mwake.

Sauti hiyo ilisikika kupitia mitandao ya kijamii. Yahya Jammeh alikuwa akizungumza kwa njia ya simu na afisa wa chama chake. Katika mazungumzo hayo,

Kufikia sasa, hakuna jipya ambalo limekwisha fanyika, kwani sauti zake nyingi zilizorekodiwa, ambazo zilivuja, zilisikika akitoa ushauri kwa chama chake cha siasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.