Pata taarifa kuu
CAMEROON-CORONA-AFYA-HAKI

Cameroon: Rais Paul Biya atangaza kuachiliwa kwa wafungwa

Rais wa Cameroon Paul Biya ametangaza kuachiliwa huru kwa wafungwa ambao hakutaja idadi, hatua ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa.

Moja ya Jela jijini Yaoundé (picha ya kumbukumbu).
Moja ya Jela jijini Yaoundé (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja katika muktadha uliowekwa katika siku za hivi karibuni baada ya baadhi ya mashirika ya kiraia na vyama vya siasa kutoa wito wa kuwaachilia huru wafungwa, ambao wanakabiliwa na hatari ya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19.

Hata hivyo idadi ya wafungwa wanaotarajiwa kuachiliwa huru haijajulikana.

Agizo la Paul Biya, lililosomwa kwenye redio ya taifa, haionyeshi idadi ya watu watakaoachiliwa huru.

Hata hivyo tangazo hilo limebaini kwamba wafungwa waliopatikana na hatia ya ufisadi, ubadhirifu au ugaidi, agizo hilo haliwahusu.

Kwa hivyo, wafungwa wanaoitwa "wa kifahari" , waliofungwa katika muktadha wa mapambano dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, agizo hilo haliwahusu". Pamoja na wote waliopatikana na hatia katika machafuko yaliyotokea katika maeneo wanakozungumza Kiingereza na ambao kwa sehemu kubwa walikataa rufaa dhidi ya hukumu yao.

Wakili Alice Nkom amesema kuridhishwa na agizo hilo, kwani, 70% ya wafungwa katika magereza ya Cameroon agizo hilo haliwahusu.

Kutokana na agizo hilo watu kati ya 2000 hadi 3000 wataachiliwa huru, kwa mujibu wa Maximilienne Ngo Mbe kutoka shirikisho la wanaharakati wa haki za binadamu katika ukanda wa Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.