Pata taarifa kuu
LIBYA-MISRI-USALAMA

Vita vya maneno vyaibuka kati ya Tripoli na Misri

Serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa imelaani kile ilichokitaja kuwa ni matamshi ya vitisho vya Vita dhidi ya Libya yaliyotolewa na rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi.

Picha kutoka ikulu ya rais wa Misri inaonyesha rais Abdel Fattah al-Sisi (katikati), Marshal Khalifa Haftar (kulia) na Spika wa Bunge la Libya Aguila Saleh (kushoto) wakiwasili kwa mkutano na waandishi wa habari mjini Cairo, Juni 6 2020.
Picha kutoka ikulu ya rais wa Misri inaonyesha rais Abdel Fattah al-Sisi (katikati), Marshal Khalifa Haftar (kulia) na Spika wa Bunge la Libya Aguila Saleh (kushoto) wakiwasili kwa mkutano na waandishi wa habari mjini Cairo, Juni 6 2020. PrΓ©sidence Γ©gyptienne/AFP
Matangazo ya kibiashara

Vita hivi vya maneno kati ya Libya na Misri vimejitokeza siku mbili kabla ya kufanyika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa ya Kiarabu kupitia mfumo wa Vidio ambao ulipangwa kufanyika Jumatatu hii, na baadaye ukaahirishwa hadi Jumanne ya juni 23 kutokana na sababu za kiufundi, kwa mujibu wa duru za kidiplomasia.

Akizungumza punde baada ya kukikagua kituo cha jeshi la wanamaji, kilichoko karibu na eneo la mpakani kati ya Misri na Libya mwishoni mwa juma lililopita, Rais wa Misri, Abdel Fattah al Sisi alisema kuwa nchi yake ina haki ya kuingilia moja kwa moja katika mzozo unaolikumba taifa jirani la Libya.

Kauli hii ya rais Al Sisi imechukuliwa na serikali ya Libya kuwa tishio la kuishamblia Libya ambapo Msemaji wa jeshi la Libya (GNA) Mohammed Gununu, ameandika kwenye mtandao wa Twitter akimjibu rais wa Misri kwamba: β€œLibya haijawahi kutishia usalama wa nchi jirani, na kwamba wako tayari kujibu mashambulkizi yoyote kutoka nje ya taifa hilo”.Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.