Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MISRI-SUDANI-USHIRIKIANO

Mvutano kati ya Ethiopia, Misri na Sudan kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile waendelea

Wakati huu Misri,Ethiopia na Sudan wakipambana kusuluhisha mzozo wa matumizi ya maji ya mto Nile, raia wa nchi hizo sasa wamepeleka mzozo huo kwenye mitandao ya kijamii.

Bwawa kubwa la Grande Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015.
Bwawa kubwa la Grande Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kwa karibu miaka 10 nchi hizo zimevutana na kushindwa kuafikiana kuhusu ujenzi wa bwawa unaotaka serikali ya Ethiopia kuanza mwezi huu.

Awali Ethiopia ilikuwa imeamua kuanza kujaza bwawa lake la mabilioni ya dola la Grand Renaissance mnamo mwezi Julai.

Misri na Sudan zote zililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita kuingilia kati mzozo huo uliodumu kwa miongo kadhaa.

Ethiopia imekuwa ikipaza sauti kuhusu nia yake ya kujaza bwala hilo, ambalo inasema ni muhimu kwa mahitaji yake ya umeme na maendeleo. Inasema mradi huo wa bwawa la umeme wenye thamani ya dola bilioni nne, utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 6,450 na utasidia kuwaondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye dimbwi la umaskini.

Misri kwa upande mwingine, inautegemea mto Nile kwa asilimia 97 ya mahitaji yake ya maji safi. Inasema bwana hilo linaweza kupunguza ugavi wake wa maji na kuwa athari mbaya kwa wakaazi wake. Sudan pia inategemea mto Nile kwa ugavi wa maji na imetoa mchango muhimu katika kuzileta pande mbili pamoja.

Misri na Ethiopia zote zilikuwa megusia uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi kulinda maslahi yao, na kuibua hofu ya kutokea kwa mgogoro wa wazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.