Pata taarifa kuu
LIBYA-MISRI-USALAMA

Libya: GNA yajaribu kuboresha maridhiano na Misri

Suala la Libya linajadiliwa kwa wiki kadhaa katika miji mikuu kadhaa ya kimataifa. Lengo: kupata suluhisho kwa mgogoro unaoendelea nchini humo.

Rais wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi akiwa na viongozi wa makabila kutoka Libya kwenye mkutano huko Cairo, Julai 16, 2020.
Rais wa Misri Abdel Fattah Al-Sisi akiwa na viongozi wa makabila kutoka Libya kwenye mkutano huko Cairo, Julai 16, 2020. Présidence égyptienne / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya majadiliano wiki hii huko Bouznika nchini Morocco na huko Geneva kati ya maafisa wa Libya kutoka kambi mbili hasimu, hatimaye mikutano inafanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo, na ujumbe wa viongozi 10 kutoka Magharibi mwa Libya wanaounga mkono serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) inayotambuliwa na jamii ya kimataifa.

Kulingana na vyanzo vyetu, mazungumzo ambayo yatafanyika hadi Jumapili, Septemba 13 yanafanyika katika "mazingira mazuri" na yanalenga kurudisha uhusiano na Misri, mshirika mkubwa wa Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya.

"Ushirikiano huu na Misri sasa unafanyika kwa sababu mambo kwa sasa ymebadilika," Saad Benshrada, mmoja wa wajumbe na afisa wa Baraza Kuu la Serikali nchini Libya amemwambia Houda Ibrahim, wa wa kitengo cha RFI katika ukanda wa Afrika (RFI Afrique).

"Walibya pamoja na jamii ya kimataifa wanaona kuwa hakuna upande katika mapambano unaoweza kushinda mwingine kwa kwa kutumia silaha. Mazungumzo pekee ndi yamesalia kama njia ya kuiokoa Libya, " ameongeza.

Saad Benshrada amesema ana matumaini kwamba "Misri, kwa kuwa ina uhusiano na Marshal Khalifa Haftar na Aguila Saleh [Spika wa bunge la Libya] inaweza kuwashawishi wawili hao ili kufikia mkataba wa kudumu wa kusitisha vita, kuanza tena uzalishaji wa mafuta na kukubali matokeo ya majadiliano yoyote kati ya Walibya katika siku zijazo”.

Kufunua ukurasa mpya

"Tunajua kwamba Misri ni nchi muhimu kwa Libya na kwamba hakutakuwa na suluhisho kwa nchi yetu bila kuishirikisha Cairo," Saad Benshrada amebaini. Tumewaambia lawama zetu lakini zilikuwa shutuma kati ya ndugu. Majadiliano yetu ni mazuri. Sisi sote tunataka kufunua ukurasa mpya na kufikiria juu ya siku zijazo. Tumeitaka Misri kudumisha mawasiliano na Magharibi mwa Libya na WaLibya wote kote nchini. Tunajua vizuri kwamba Misri ni mshirika mkubwa, hodari na mwenye nguvu katika Mashariki ya Kati. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.