Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

KNK yafutilia mbali shutma dhidi ya Bozizé kama kiongozi wa waasi

Wakati mazungumzo yakiendelea kati ya wajumbe wa ECCAS, Jumuiya ya Mataifa ya Afrika ya Kati na viongozi kadhaa wa waasi, ikiwa ni pamoja na François Bozizé, chama cha rais huyo wa zamani kimekanusha uhusiano wa kiongozi wake na muungano wa makundi ya waasi.

KNK yafutilia mbali shutuma dhidi ya  François Bozizé kama kiongozi wa waasi.
KNK yafutilia mbali shutuma dhidi ya François Bozizé kama kiongozi wa waasi. Gaël Grilhot
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, chama cha KNK cha François Bozizé, kinasema kiongozi wake hana uhusiano wiwote na muungano wa makundi ya waasi (CPC), uliovuruga mchakato wa uchaguzi na kujaribu kuingia katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, Januari 13.

 

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, chama cha François Bozizé kinashtumu serikali kwa kumchukulia kiongozi wake kama mwanzilishi wa muungano wa makundi ya waasi, na ambaye anahusika na uhalifu uliotekelezwa na makundi hayo.

 

Wito wake wa kususiwa kwa uchaguzi wa mwezi Desemba na kuunga mkono msimamo wa kiitikadi wa waasi, haupaswi kuchukuliwa kama yeye ndio kiongozi wa muungano huo, chama cha KNK kimebaini.

 

Taarifa hiyo kwa waandishi wa habari iliyosainiwa na msemaji wa chama hiki Christian Guénébem, inalaani kuanzishwa kwa mapigano, na kufutilia mbali mashtaka dhidi ya kiongozi wake, huku kikibaini viongozi wa muungano huo wa makundi ya waasi walimuona Bw. Bozizé na kumtaka kushirikiana nao lakini " bado hajawajibu "

 

Lakini, kwa sauti ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Jumanne jioni, François Bozizé alisikika akiwataka wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kuunga mkono muungano wa makundi ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.