Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Save the yalaani ukatili unaofanyiwa watoto Cabo Delgado

Shirika la Kimataifa linalotoa misaada la Save the Children, linasema majihadi wanawauwa watoto kwa kuwakata vicha katika jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji

Mwanamke, anayeitwa Elsa na shirika la kutoa misaada la Uingereza la Save the Children, amesimama na familia yake katika kambi ya wakimbizi wa ndani kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji.
Mwanamke, anayeitwa Elsa na shirika la kutoa misaada la Uingereza la Save the Children, amesimama na familia yake katika kambi ya wakimbizi wa ndani kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado, Msumbiji. via REUTERS - Rui Mutemba/Save the Children
Matangazo ya kibiashara

Mama mmoja, ameliambia Shirika la Save the Children kuwa, alishuhudia kwa macho yake, mtoto wake wa kiume wa miaka 12 akiuawa  kwa kukatwa kichwa, karibu na eneo ambalo alikuwa amewaficha watoto wake wengine.

Katika ripoti yake, Shirika la Save the Children limesema kuwa limekuwa likizungumza na familia za watoto ambao wameuawa katika jimbo la Cabo Delgado lenye utajiri wa gesi na mbali na mauaji hayo, makaazi ya familia mbalimbali, yameteketezwa moto.

 Umoja wa Mataifa umesema mauaji yanayoshuhudiwa Kaskazini mwa Msumbiji hayawezi kuelezwa hasa baada ya magaidi hao wanaoshirikiana na kundi la Islamic State kuanza kuwashambulia watoto.

 Kundi hilo linalofahamika kama Al Shabab, limesababisha maafa ya watu 2500 na wengine 700,000 wameyakimbia makwao tangu mwaka 2007.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.