Pata taarifa kuu
MISRI

Misri: Juhudi zaendelea kuondoa meli iliyokwama kwenye mfereji wa Suez

Meli 100 zimekwama kwenye mfereji wa Suez, nchini Misri baada ya  meli moja kubwa kuharibika na kukwamisha shughuli zote kwenye bandari hiyo.

Misri imesema imefungua njia ya zamani kugeuza mkondo wa meli zingine ili kuzuia msongamano, huku kukiwa na wasi wasi njia ya sasa itazibwa kwa siku kadhaa.
Misri imesema imefungua njia ya zamani kugeuza mkondo wa meli zingine ili kuzuia msongamano, huku kukiwa na wasi wasi njia ya sasa itazibwa kwa siku kadhaa. VIA REUTERS - Suez Canal Authority
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa mamlaka katika mfereji wa Suez, hiyo Admiral Osama Rabie, amesema  juhudi zinaendelea za kuondosha meli hiyo iliyoharibika, ambayo ametaja kuwa meli kubwa zaidi kuwahi kukwama.

 

Boti za kuvuta na wachimbaji wanafanya kazi ya kuisaidia meli kubwa ya kontena kuelea tena majini baada ya meli hiyo kuziba mfereji wa maji wa Suez nchini Misri, moja wapo ya njia zenye shughuli za biashara ulimwenguni.

 Wamiliki wa meli hiyo yenye urefu wa mita 400 sawa na (futi 1312) wanasema ilikwama upande mmoja baada ya kupigwa na upepo mkali.

Misri imesema imefungua njia ya zamani kugeuza mkondo wa meli zingine ili kuzuia msongamano, huku kukiwa na wasi wasi njia ya sasa itazibwa kwa siku kadhaa.

Tukio hilo tayari limesababisha msongamano wa majini huku baadhi ya meli zikikosa njia ya kupita ambapo Karibu asilimia 10 ya biashara duniani zinazofanywa kupitia mfereji huo wa Suez, ambao unaunganisha bahari ya Mediterrania na bahari nyekundu (Red Sea) na kutoa njia fupi ya majini kati ya Asia na Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.